AyoTV

Haji Manara kaiomba TFF iipe Simba SC kombe mbele ya Sevilla

on

Club ya Simba SC May 23 2019 itacheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya club ya Sevilla ya nchini Hispania uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, game hiyo ikiwa ya kirafiki lakini inapewa uzito mkubwa kutokana na ukubwa wa club ya Sevilla.

Kuelekea mchezo huo Haji Manara leo mbele ya waandishi wa habari ameongea na kuiomba shirikisho la soka Tanzania TFF, kuwa kama watakuwa wametangazwa Mabingwa wa ligi Kuu siku hiyo basi anaomba wakabidhiwe kombe lao mbele ya Sevilla.

Sevilla ni Mabingwa wa Kombe la Europa League mara tatu mfululizo wakati huo wakifundishwa na kocha wa sasa wa Arsenal Unai Emery (2014,2015, 2016), wakati hadi sasa wakiwa nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania LaLiga kwa kuwa na jumla ya point 55 wamecheza jumla ya michezo 36, ushindi michezo 16, sare 7 na wamepoteza jumla ya michezo 13.

Samatta kaweka historia Ubelgiji, mchezaji wa tatu kuwahi kushinda Ebony Award 2019

Soma na hizi

Tupia Comments