Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea tena leo kwa watani wa jadi Simba na Yanga kusafiri nje ya Dar es Salaam kwenda kutafuta point tatu ugenini, Yanga walikuwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar na Simba SC walikuwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga kucheza dhidi ya Coastal Union.
Bahati mbaya Yanga na Simba ambao ndio wanaopewa nafasi ya kutwaa taji hilo mmoja wao anazidi kudhoofika kwa kupoteza point, Yanga leo wamepoteza mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa goli 1-0 lililofungwa na Hamis dakika ya 52, kwa maana hivyo wamepoteza point tatu katika mbio za kuwania Ubingwa wa TPL.
Simba SC baada ya kufungwa goli la mapema dakika ya kwanza dhidi ya Coastal Union lililofungwa na Hafidh, walirudi mchezoni kipindi cha pili na kujikuta wakisawazisha na kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Simba SC yalifungwa na mshambuliaji wao raia wa Rwanda Meddie Kagere aliyefunga yote mawili dakika ya 48 na 67.
Mwana FA kakutana na Jose Mourinho uso kwa uso, kamwambia yale maneno yake?