Michezo

Jurgen Klopp kwa watakaoishangaa Liverpool miaka 30 bila EPL

on

Baada ya club ya Liverpool kuukosa Ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mwaka 29 ni wazi sasa inaelekea mwaka wa 30 bila kutwaa taji hilo, hivyo presha imekuwa kubwa kwa mashabiki wa Liverpool na kutaka kuona timu yao inatwaa taji hilo ambalo wamelikosa kwa muda mrefu.

Liverpool pamoja na kuwa wapo katika fainali ya UEFA Champions League na watacheza na Tottenham Hotspurs June 1 2019, bado wanashauku ya kutaka taji la EPL kuliko la Champions League ambalo ni kubwa zaidi ya EPL ila kutokana na hawajatwaa taji hilo kwa muda mrefu.

Baada ya kuwa wanaenda mwaka wa 30 pasipokutwaa taji hilo kocha wao Jurgen Klopp kaongea kuhusiana na wale wanaowabeza kuwa mwaka wa 30 bila taji “Watu watatwambia kuwa miaka 30 toka Liverpool itwae Ligi Kuu kwa mara ya mwisho lakini wao kiukweli wana matatizo makubwa watu wote watakaosema hivyo”

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments