Habari za Mastaa

French Montana amewajengea mjengo Ghetto Kids wa Uganda

on

Rapper French Montana kutokea Marekani ameamua kuwajengea nyumba watoto wa kundi la Ghetto Kids kutokea nchini Uganda na tayari nyumba hiyo ipo tayari.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa kundi la Ghetto Kids limemshukuru French Montana kwa kitendo alichokifanya pamoja na ku-post picha ya nyumba hiyo, ikiwa tayari imekamilika mwaka mmoja tokea kundi hilo lifahamiane na French Montana.

“Mwaka 2018 umekuwa mzuri kwetu,Tunamshukuru Mungu kwa baraka na tunaomba aendelee kutubariki zaidi na zaidi. French Montana pamoja na team nzima hatuwezi kacha kuwashukuru vya kutosha , Tunamuomba Mungu kuzidi kuwabiriki na tutazidi kujivunia kuwa na wewe , maneno hayotoshi kuelezea tulivyofurahi ila Mungi ndio anajua kilichopo moyoni kwetu”

French Montana alikutana na kundi la Gheto Kids mwaka 2017 na kuwapatia nafasi ya kucheza kwenye ngoma ya ‘Unforgettable’ na baadae walipewa nafasi ya kutumbuiza kwenye tuzo za BET 2017 nchini Marekani.

Calisah anunuliwa gari na aliekuwa mapenzini na Otile Brown, Vera Sidika

Soma na hizi

Tupia Comments