Michezo

Paul Pogba adaiwa kuigawa Man United

on

Bado headlines za kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Man United ya England Paul Pogba kudaiwa kutokuwa katika mahusiano na mazuri na kocha wake Jose Mourinho zinazidi kushika kasi.

Pogba baada ya kunaswa katika picha za video zikimuonesha kutokuwa na uhusiano mzuri na kocha Jose Mourinho kutokana na kushindwa kupeana mikono wakati wa kuanza mazoezi jana, inadaiwa kuwa Man United sasa imegawanyika makundi mawili.

Wapo baadhi ya wachezaji wa Man United wanaompinga Jose Mourinho na kumkubali Pogba na wapo wanaompinga Pogba na kumuunga mkono Jose Mourinho ila kwa sasa indaiwa kuwa Anthony Martial na Eric Bailly wanamuunga mkono Pogba hivyo ndani ya Man United kuna mgawanyiko.

JB na Ray “Hata Yanga wao wanajua Simba ana timu bora”

Soma na hizi

Tupia Comments