Maumivu ya club ya Inter Milan kutolewa hatua ya makundi katika michuano ya UEFA Champions League yamewaumiza mashabiki wengi wa soka nchini Italia akiwemo mke wa mchezaji wa timu hiyo Mauro Icardi anayejulikana kwa jina la Wanda Nala.
Wanda Nala alikuwa sehemu ya mashabiki waliyokuwa wamejitokeza Sansiro kuangalia game ya Inter Milan dhidi ya PSV, ambayo Inter Milan kama angeshinda basi angefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/19.
Inter Milan kwa bahati mbaya alilazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 na PSV, hivyo amemaliza nafasi ya tatu katika Kundi B akiwa na point nane na kuziacha Tottenham na FC Barcelona zikiingia hatua ya 16 bora, mke wa Icardi licha ya kushuhudia mmewe akifunga goli lakini halikuwa na msaada kwa Inter Milan.
Hata hivyo kwa upande wa Icardi amekuwa na msimu mzuri safari hii toka mwanzo wa msimu akicheza game 18 na kufunga magoli 12 na anahusishwa kuhama club hiyo na kujiunga na club za Real Madrid na Chelsea.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe