Mix

IMERIPOTIWA: Kondakta auwawa kwa kipigo cha Wanajeshi Tanga

on

AzamTV News imeripoti kwamba Inadaiwa Wanajeshi wamehusika kwenye mauaji ya kijana mmoja wa Tanga ambaye kazi yake ilikua ni Kondakta wa daladala.

Mmoja wa Wananchi waliohojiwa na AzamTV amesema kilichotokea ni Mwanafunzi wa kike ambaye ni mtoto wa Mwanajeshi kupanda Daladala bila kulipa nauli lakini Kondakta akachukua maamuzi ya kumzuia yule binti kwamba lazima alipe nauli.

Inadaiwa Baba mzazi wa Binti huyo ambaye ni Mwanajeshi aliagiza vijana kwenda kumkamata Kondakta na kumpeleka kwenye kambi ya Jeshi na wakampiga mpaka hali yake ikawa mbaya kisha wakamrudisha nyumbani kwake na baadae watu wakaona akichukuliwa na kupelekwa Hospitali akiwa ameshafariki.

Sehemu ya Wananchi wengine waliotoa maoni yao ni Mwanamke mkazi wa Nguvumali aliesema huyu ni mtu wa tatu anauwawa na Wanajeshi kwenye mji wa Tanga ‘Wamezidi kutuonea ndio kawaida yao… tumechoka’

Kamanda wa Polisi Tanga Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mpaka sasa watu watatu wanashikiliwa na Polisi na taratibu za upelelezi zikikamilika hatua dhidi yao za kufikishwa Mahakamani zitachukuliwa.

Tukio kufanyikia kwenye kambi ya jeshi haina maana kwamba Wanajeshi wamehusika kwasababu ndani ya kambi ya jeshi tunazo familia za Askari ambao sio Askari bali ni raia wa kawaida na ndio maana mpaka sasa tunaowashikilia kuanzia yule binti ni raia tu wa kawaida pamoja na hao wengine tuliowakamata‘ – Kamanda Wakulyamba

Kuitazama taarifa yenyewe unaweza kubonyeza play kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments