Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Wanawake Laki Moja inatarajia kufanya kongamano la kwanza la Wanawake na Utalii lenye lengo la kumkomboa Mwanamke katika nyanja mbalimbali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Msaidizi wa Taasisi hiyo Nangasu Warema amesema kongamano hilo halijawahi kutokea na lengo ni kumkomboa Mwanamke kiuchumi.
“Kongamano litakuwa kubwa na halijawahi kutokea, tunataka tumpe Mwanamke mafunzo na ajikomboe dhidi ya ukatili, sekta ya utalii ina mambo mengi hivyo itakuwa fursa endapo tukiitumia vyema kwani kwa mujibu wa takwimu inaonyesha kuanzia mwezi January hadi July sekta hiyo imekuwa kwa asilimia 62.7”- Nangasu Warema