Michezo

Taarifa rasmi ya Ryan Giggs kustaafu soka

on

1966912_730304170366864_4292087558580139743_nMuda mfupi baada ya kutangazwa kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Manchester United, mwanasoka Ryan Giggs ametangaza rasmi kustaafu soka.

Giggs ambaye alianza kuichezea timu ya watoto ya Manchester United mwaka 1991, amestaafu soka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 23 huku akifanikiwa kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika klabu yake ya Manchester United ambazo ni 963.

Giggs anastaafu akiwa ndio mwanasoka ambaye kashinda makombe mengi zaidi, 13 ya premier league, FA Cup 4, Capital One 4, mawili ya kombe la klabu bingwa ya ulaya na 2 klabu bingwa ya dunia, pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa ligi mara mbili mwaka 1992 na 1993, pia alishinda tuzo hiyo kutoka kwa klabu ya Manchester United mwaka 1991 na 1992. 

Mwaka 2009 alishinda tuzo ya BBC Sports Personality of the year na pia akashinda PFA Player of the year award na ametajwa kuwa mchezaji bora mara 6. 

Tupia Comments