Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa fomu za uteuzi kwa wagombea wa kiti cha Rais na
Makamu wa Rais wa vyama kumi na sita (16) vya siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Agosti 11, 2020, Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume, Dkt. Wilson Mahera Charles amesema fomu kwa wagombea hao
zimetolewa kuanzia Agosti 5, 2020.
Dkt. Mahera amesema kwamba wagombea hao wanatarajiwa kurejesha fomu hizo Agosti 25, 2020 kwa ajili ya uteuzi ambao utafanyika siku hiyo.