Top Stories

Taarifa ya CHADEMA kumhusu Mbwana Samatta “Serikali itumie fursa” (+video)

on

CHADEMA imetoa pongezi kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta kwa kufanikiwa kuwa Mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza Ligi Kuu ya Uingereza, akisajiliwa katika klabu ya Aston Villa kwa mkataba wa miaka 4 na nusu.

“CHADEMA inamtakia kila la heri Samatta ili mafanikio yake ya kucheza kwenye mojawapo ya Ligi kubwa Duniani yawe chachu na hamasa kubwa ya kuongeza mori na bidii ya kusonga mbele zaidi, kwake yeye na wachezaji wa Kitanzania, wanaocheza ndani na nje ya Nchi yetu”– CHADEMA

“Tunatoa wito kwa Serikali kuitumia kwa haraka milango ambayo itakuwa imefunguka au fursa zilizotengenezwa kupitia Samagoal kusajiliwa na Aston Villa”-CHADEMA

BREAKING: TCRA WATANGAZA HABARI MPYA “HATUTAZIMA LAINI ZOTE AMBAZO HAZIJASAJILI LEO

Soma na hizi

Tupia Comments