Top Stories

Taarifa ya Serikali juu ya vifo vya samaki Ziwa Victoria

on

Mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka 2021, kulitolewa taarifa ya vifo vya samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria nchini Uganda, hasa katika maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo. Samaki waliokufa katika tukio hili ni aina ya sangara wakubwa.

Baada ya kupata taarifa hizi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikishirikiana na Taasisi yake ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kituo cha Mwanza iliwasiliana na maafisa uvuvi, wavuvi, na wadau wengine wa uvuvi katika Ziwa Victoria eneo la Tanzania, kikiwemo Chama cha Wavuvi Tanzania (TAFU).

Ufuatiliaji wetu umeonyesha kuwa upande wa Tanzania, vifo hivi havijaripotiwa sehemu yoyote isipokuwa kwa wavuvi na wananchi wa eneo la Masonga – Sota, Tarime ambao walidai kuona vifo vya samaki siku ya Jumamosi tarehe 2, Januari 2021.

Hata hivyo maafisa uvuvi wa eneo husika hawakuona samaki waliokufa katika siku iliyotajwa na hata baada ya siku chache
zilizofuatia.

Maeneo mengine yote ya ziwa upande wa Tanzania hakukuwa na taarifa za vifo. Maeneo hayo ni Malei mpakani na Uganda, Bukoba, Misenyi, visiwa vya Ukerewe na Gozba, Busekela – Musoma, Nyamikoma – Busega na maeneo ya Mwanza na Muleba.

VITA YA MAJOGOO, SABABU ZA WAO KUPIGANA KUUTAKA UTAWALA WA ENEO

Soma na hizi

Tupia Comments