Moja kati ya habari kubwa kwa sasa Tanzania ni kuhusiana na usajili wa mshambuliaji Vipers SC ya Uganda Raia wa Congo DR Cesar Manzoki (25) ambaye amekuwa akihusishwa na Simba SC kwa muda mrefu kiasi cha wengi kuamini kuwa alikuwa njiani kuelekea Misri Ismaily kuungana na timu ambako imeweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya.
millardayo.com imefuatilia kwa kina ukweli wa tetesi zilizopo kutoka chanzo cha ndani nchini Uganda ni nini kinachelewesha dili la Manzoki kujiunga na Simba SC na kweli Simba wanamuhitaji au ni tetesi tu, kwa mujibu wa mtangazaji wa michezo na afisa mahusiano wa NBS TV za nchini Uganda Desire Derekford Mugumisa ametoa ufafanuzi wa kina kuhusiana kinachoendelea kati ya Manzoki na club yake ya Vipers.
Kupitia twitter account yake Mugisa ameeleza kuwa Simba na Manzoki washakubaliana na kusaini mkataba wa awali yaani Pre Contract hivyo Manzoki atajiunga na Simba SC ila lini ndio changamoto, Manzoki bado ana mkataba na Vipers hadi October 2022 yaani mkataba wake umesalia miezi miwili na nusu ila Vipers wamegoma kumuachia licha ya Manzoki na meneja wake kutaka kununua miezi michache iliyosalia ila Vipers wameweka ngumu.
Baada ya Vipers kuweka ugumu Manzoki na mwanasheria wake wameandika barua FIFA ya kutaka waingilie kati suala hilo kwani mchezaji anataka kuondoka, FUFA wameamua kuingilia kati kabla ya FIFA na wanaamini kuwa watatatua changamoto hiyo ila Manzoki leo amehudhuria mazoezi ya timu yake kama kawaida na kuendelea kuheshimu mkataba wake ila kwakuwa ana mkataba wa awali na Simba SC basi Manzoki atajiunga na Simba SC mara baada ya kumalizana na Vipers kwa namna yoyote.
Kama utakuwa humfahamu vizor Cesar Manzoki ni mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Uganda 2021/2022, mfungaji bora wa Uganda akiwa na magoli 18 2021/2022, mchezaji bora wa wachezaji na mshambuliaji bora wa msimu, Cesar Manzoki amewahi kucheza Timu ya Taifa ya Congo DR 2016 kwa mechi 3 na 2022 akaanza kuitumikia timu ya Taifa ya Afrika ya Kati kwa lugea rahisi ana Uraia wa nchi mbili.