Michezo

Taarifa zaidi ya ajali ya Kobe Bryant na Binti yake Gianni

on

Ajali ya Kobe Bryant ya helikopta yake binafsi yenye namba N72EX iliyotokea jana na kudaiwa kuwa imeua watu watano taarifa rasmi sasa zinaeleza ilikuwa na jumla ya watu 9 akiwemo Kobe Bryant ,41, na binti yake Gianni Maria-Onore ,13, rubani wa zamani wa Kobe Bryant ajulikanae Kurt Deetz aeleza kuwa helikopta ya Kobe ni miongoni wa helikopta ghali na salama zaidi duniani.

Mkuu  wa ulinzi wa Los Angeles Sherrif Alex amethibitisha kuwa ajali hiyo imehusisha jumla ya watu tisa na hakuna hata mmoja aliyenusurika, taarifa zaidi zinaeleza kuwa mamlaka ya usalama imesema itatoa majina rasmi ya waliofariki baada ya familia ya marehemu hao kupewa taarifa.

Ni wazi ajali hiyo watu waliofariki waliokuwa wanaelekea katika kituo cha Basketball wamefikia watano kutokana na familia ya kocha wa mchezo wa kikapu kutoka chuo cha Orange Coast John Altobelli, mkewe Keri Altobelli na mtoto wao Alyssa Altobelli kuthibitisha kuwa hao pia walikuwepo kwenye helikopta hiyo.

VIDEO: RAHA ILIYOJE !!! BABA MZAZI WA SAMATTA, HAKULALA ANACHEZA MUZIKU UTAMBULISHO WA ASTON VILLA

Soma na hizi

Tupia Comments