Taasisi ya Flaviana Matata Foundation(FMF) ambayo inafanya kazi ya kukwamua ndoto za mtoto wa kike ili aweze kufika katika malengo yake,Leo wametembelea shule ya secondari ya wasichana Mandela iliyopo wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani kwa lengo la kutoa elimu na kuwasikiliza wanafunzi hao wa kike changamoto wanazopitia katika elimu na pia changamoto wanazopitia katika jamii zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa programu Bi Suzan Cleophas amesema ” Lengo la kutembelea shule hii ni kuongea na wasichana hawa kuhusu umuhimu wa kusimamia ndoto zao, kuwakumbusha wao ni wakina nani katika jamii, kawaelemisha kuhusu kujitambua na kujiamini, kusikiliza kero na changamoto wanazo kumbana nazo katika masomo yao na mwisho umuhimu kuhusu elimu sahihi ya hedhi salama”.
Kupitia shughuli ya satellite katika shule ya secondary Mandela, wamewafikia wanafunzi takribani 512 watokao kata mbalimbali za mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.
Mwisho afisa programu huyo amesema kuwa “wameendelea kuwakumbusha walimu kuwa nao wana nafasi kubwa ya kuhakikisha mtoto wa kike anabaki shule, kuongeza ufaulu na pia mtoto wa kike anafikia ndoto zake kwa Elimu aipatayo”.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi Flora Sereto ameeleza kuwa “changamoto wanazopitia na kuwafanya wasitishe masomo ni pamoja na Mila na Utamaduni wa Mkoa huo wa Pwani na kusema zinawarudisha nyuma hasa Wanafunzi wakike kwani Ulazimishwa ndoa za utotoni na ndio sababu kubwa ya wengi wao kuacha masomo.”
Mwisho,tunaishukuru taasisi ya FMF kwa kutuapatia elimu ya hedhi salama na kutupa pedi kwasababu ni changamoto kubwa ambayo wengi wao wanaipata wakiwa shuleni.”