Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Taasisi ya Hassan Maajar yakabidhi darasa la Kompyuta Shule ya Majengo
Share
Notification Show More
Latest News
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kurejelea kesi yake na tuhuma za ufisadi
December 4, 2023
Marekani imeingilia kinyume cha sheria bahari ya Kusini -China
December 4, 2023
Haaland anaweza kukabiliwa na hatua ya kinidhamu
December 4, 2023
Sitaki kuitazama Man United tena-Gary Neville
December 4, 2023
Newcastle wanapaswa kumsajili David De Gea ili kuziba pengo la Nick Pope
December 4, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Mix > Taasisi ya Hassan Maajar yakabidhi darasa la Kompyuta Shule ya Majengo
Mix

Taasisi ya Hassan Maajar yakabidhi darasa la Kompyuta Shule ya Majengo

November 17, 2023
Share
5 Min Read
SHARE

Taasisi ya Hassan Maajar Trust (“HMT”), imeendeleza dhamira yake ya kuboresha mazingira ya shule za msingi nchini, ambapo leo imekabidhi darasa la kompyuta pamoja na kompyuta kumi na tatu (13) kwa shule ya msingi Majengo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani. Jengo hilo lililogharimu jumla ya Shillingi milioni Thelathini na Mbili 32,000.00 na Dola 10,000.00 kwa ajili ya kompyuta kumi na tatu zilizofadhiliwa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVep) inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.

Gharama za ujenzi ni kubwa kidogo kwa kuwa shule haina uzio hivyo ikabidi kuweka madirisha imara ili kulinda kompyuta zitakazokuwa darasani.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Maajar, alikabidhi darasa na kompyuta hizo kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bi. Magdalena Tiothem Amsi katika hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki na iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimiwa Bi Halima Okash, ambaye alikuwa mgeni rasmi, wawakilishi wa Barrick, Maofisa kutoka Kitengo cha elimu , walimu na wanafunzi.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash, ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi, aliipongeza, HMT, kwa kuamua kuzikabili changamoto za kuboresha mazingira ya elimu kwa kutoa misaada ya madawati, huduma za maktaba, kujenga miundombinu ya vyoo na sasa darasa la kompyuta pamoja na kompyuta kwa shule ya Msingi Majengo. “Kwa niaba ya serikali nawapongeza kwa jitihada mnazofanya kuboresha mazingira ya kupata elimu mashuleni” alisema.

Akiongea katika hafla hiyo, Balozi Maajar alisema “Hii ni sehemu ya utaratibu wa taasisi ya HMT kuasili shule na kubaki hapo kufanya ujenzi au ukarabati wa majengo na miundo mbinu ya kusomea hadi ikiwa imetangamaa ndiyo wanaondoa uasili”. Kwa sasa wanaendelea kuomba wabia kushirikiana kufanya ukarabati mkubwa wa madarasa 5 hapo shuleni Majengo.

Aidha alisema kuwa “kwa kipindi kirefu nyuma, HMT ilikuwa inajulikana kwa kampeni yake kubwa ya ‘Dawati Kwa Kila Mtoto’ ambayo imefanikiwa kwa kutoa madawati 10,000, na kunufaisha Zaidi ya wanafunzi 30,000 katika mikoa 13 nchini. Tuliona vilevile kuna haja ya kufundisha elimu ya kompyuta shule zetu za msingi kwa sababu ni jambo lisilokwepeka katika muktadha wa dunia ya leo. Aidha alisema, kila safari ni hatua ya kwanza na kwa mradi huu ndiyo hatua ya kwanza kwa HMT kutimiza lengo la kuiborehsa shule hii iliyoiasili ili ipate kuwa mfano wa kuigwa kwa wafadhili na watu wenye nia njema kuunga juhudi za Serikali katika kuboresha elimu nchini”.

Alisema Kupitia hafla tofauti za ukusanyaji fedha kama vile ‘Fundraising Gala’ na ‘Matembezi ya Hiyari’, HMT kupitia kampeni ya Dawati kwa Kila Mtoto ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhamasisha umma kuona kuwa wajibu wa kuboresha mazingira ya shule zetu si wa Serikali pekee na kuweza kuchangia madawati mengi lakini changamoto hii bado ipo kutokana na ongezeko la wanafunzi baada ya seara ya Serikali ya elimu bure kwa kola mtoto. Kwa HMT ni faraja kubwa kuona idadi kubwa ya watoto wetu siku hizi wakiwa hawakai tena chini.

Mwakilishi wa Barrick katika hafla hiyo, Georgia Mutagahywa, alisema kuwa NVep na Barrick imeona fahari kushirikiana na HMT katika mradi huu kwa kuzingatia umuhimu wa suala la TEHA katika shughuli nyingi za kazi na maendeleo ya mtu binafsi na nchi kw aujumla. Barrick inatambua umuhimu wa Watoto kuanza kujifunza masuala ya TEHAMA mapema na imefurahi kupata fursa ya kuchangia katika jambo hili muhimu.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Majengo, Bi. Magdalena Tiothem Amsi, aliishukuru taasisi ya HMT kwa kutoa msaada huo ambao alisema “utawezesha wanafunzi wa shule hiyo kusomea katika mazingira rafiki na hasa kwa hili darasa wanfunzi wa Majengo wataweza kuwa na elimu ya TEHAM ambayo kwa sasa ni muhimu sana duniani kote”, alisema.

Taasisi ya Hassan Maajar inafanya maandalizi ya kukarabati madarasa 5 hapo shuleni Majengo na wanaomba wafadhili na wabia wao kusaidia kuchangia kutimiza lengo hilo.

HMT ina imani watu wengi wataendelea kuhamasika kushiriki kwa kutambua kuwa ni jukukumu letu sote kuborehsa mazingira ya kusomea kwa watoto wetu ambao ndiyo taifa la kesho na siyo tu kazi ya serikali peke yake.

You Might Also Like

Wanafunzi wazidi kunufaika na elimu ya kupinga ukatili

Mgodi wa Barrick Mara kinara kodi ya Mauzo ya nje

Serengeti waunga mkono usawa wa kijinsia

Ditto Mahakamani kudai fidia ya Tsh Bilioni 6

Makamu wa Rais wa Yanga ashinda tuzo ya CEO Bora UK

Rama Mwelondo TZA November 17, 2023
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Yanga SC kwenye viwango vya klabu bora Duniani yashika namba 4 huku mpinzani wake Simba namba 12
Next Article Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 17, 2023
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kurejelea kesi yake na tuhuma za ufisadi
Top Stories December 4, 2023
Marekani imeingilia kinyume cha sheria bahari ya Kusini -China
Top Stories December 4, 2023
Haaland anaweza kukabiliwa na hatua ya kinidhamu
Sports December 4, 2023
Sitaki kuitazama Man United tena-Gary Neville
Sports December 4, 2023

You Might also Like

Top Stories

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kurejelea kesi yake na tuhuma za ufisadi

December 4, 2023
Top Stories

Marekani imeingilia kinyume cha sheria bahari ya Kusini -China

December 4, 2023
Sports

Haaland anaweza kukabiliwa na hatua ya kinidhamu

December 4, 2023
Sports

Newcastle wanapaswa kumsajili David De Gea ili kuziba pengo la Nick Pope

December 4, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?