Taasisi ya Taawanu Islamic Foundation chini ya Mkurugenzi wake wa Kimataifa Hajjat Zahra Dattan (zaradattani on Instagram) imeendelea na zoezi la ugawaji wa vitanda vya kisasa ambapo leo ilikuwa ni zamu ya Wilaya ya Kyerwa iliyopo Mkoani Kagera.
Kiongozi huyo wa Kimataifa akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Taawanu Tanzania na Afrika Sheikh Hashimu Kamugunda pamoja na Viongozi wengine wa Taasisi hiyo ngazi ya Mkoa na Taifa wamefika katika Wilaya ya Kyerwa kwenye zahanati ya Katera kwa ajili ya kutoa msaada wa vitanda kwa ajili ya kuongeza nguvu ya utoaji huduma katika zahanati hiyo.
Akiongea kwa niaba ya taasisi hiyo Hajjat Zahra amesema kuwa wametoa msaada huo baada ya kupokea maombi kutoka kwa wadau ambao waliona zoezi la uzinduzi wa ugawaji wa vitanda 60,000 Kitaifa ndo akaamua afike katika zahanati hiyo ya Serikali iliyojengwa kwa mchango wa wananchi na serikali kwa ajili ya kukabidhi vitanda hivyo pamoja na kuangalia ni namna gani wanaweza kusaidia upande mwingine kwa kushirikiana na serikali ili wananchi waendelee kupata huduma iliyo bora.
Aidha Hajjat Zahra amewaomba wasimamizi na wananchi watakaotumia vitanda hivyo kuvitunza vizuri ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia walio wengi.
Sambamba na hilo amekabidhi mitungi ya gesi kwa baadhi ya akina mama wa eneo la Katera ikiwa ni hamasa ya kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia ambayo itawaepusha na changamoto nyingi za Kiafya.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa,Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Daktari Lewanga Msafiri Mandari ameshukuru taasisi ya TAAWANU kwa msaada mkubwa walioutoa katika Wilaya hiyo huku akisema kuwa vitanda walivyovipokea ni vya kisasa na kipekee kabisa ndani ya Wilaya yao kwani ndo mara ya kwanza kupokea vitanda vyenye muundo kama huo na anaamini vitawasaidia kupunguza uchovu kwa watoa huduma pamoja na wauguzi kwani vinatumia teknolojia ya kisasa