Habari za Mastaa

Drake alivyompandisha Wizkid stejini (+video)

on

Rapper Drake akiwa katika ziara yake ya ‘Assassination Vacation’ jijini London Uingereza  amempandisha kwenye stage Wizkid ambaye wamewahi kufanya kazi pamoja kwenye mdundo wa  ‘Come Closer’ pamoja na ‘One Dance’ na kutumbuiza kwa pamoja ngoma hizo.

Inasemekana kuwa Drake na Wizkid wameonana kwa mara ya kwanza usiku huo baada ya kuwahi kusambaa kwa taarifa kuwa wawili hao walikuwa hawaelewani ambapo maneno mengi yalizuka na kuhusisha kuwa ni kuhusu ngoma yao waliofanya pamoja lakini kwa upande wao hawakuwahi kuzungumza chochote kuhusu hilo.

Drake akiwa bado kwenye stage, Wizkid alipata nafasi ya kujimwaga na ngoma zake kibao ikiwa pamoja na ngoma yake ya ‘Soco’ na nyingine nyingi.

VIDEO: LULU DIVA KUOLEWA/ AROBAINI YA RUGE/ ALIKIBA AMUONYESHA MTOTO WAKE

Soma na hizi

Tupia Comments