Top Stories

Taharuki uwanja wa Ndege, abiria wakimbia ‘Tishio la usalama wa bomu’

on

Baada ya kutokea kwa taharuki uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (Terminal 2), Dar es salaam mapema leo, Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja huo amesema kilichotokea ni zoezi la kujiwekea tayari endapo kutatokea majanga na kusema zoezi hilo limepangwa kwa siri bila Abiria wala wadau wengine kujua.

Sasa Uongozi wa Uwanja wa Ndege umetoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari…“Tulichokifanya leo ni kwamba ni kama vile tumepata taarifa za uwepo wa bomu kwenye ukumbi wa abiria na tukawahi kuokoa, tunaomba Wananchi waondoe hofu hili ni zoezi la kawaida hakuna kilichotokea”

Soma na hizi

Tupia Comments