Michezo

Taifa Stars yakabidhiwa Milioni 60, kila la heri michuano ya CHAN 2021

on

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega akimkabidhi nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Taifa ( Taifa Stars) John Bocco fedha za posho za ndani za wachezaji pamoja na bonasi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DRC ikiwa ni sehemu ya mchango wa Serikali kusaidia maandalizi ya timu hiyo kuelekea mashindano ya CHAN 2021 nchini Morocco.

Katika hafla ya kuiga timu hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hotel ya Tiffany jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Ulega pia aliwakabidhi viongozi pamoja na wachezaji wa timu bendera ya Taifa.

“Serikali imechangia zaidi ya shilingi Milioni 60 kama bonasi na posho za ndani za wachezaji na benchi la ufundi, bado tunapambana kupata fedha ili kusaidia katika maeneo mengine, TFF hakikisheni mnasimamia nidhamu ya matumizi ya fedha hizi pamoja na nidhamu kwa vijana ili timu yetu iweze kutuwakilisha vyema” alisisitiza Mhe. Ulega.

Taifa Stars imeondoa leo alfajiri kuelekea nchini Morroco kushiriki michuano ya CHAN 2021.

 

Tupia Comments