Michezo

Kilichoikuta Taifa Stars kwenye mechi dhidi ya Burundi hiki hapa

on

stars-1Timu ya taifa ya Tanzania leo ilikuwa jijini Bujumbura Burundi kukupiga na timu ya taifa ya nchi hiyo kwenye mchezo wa kirafiki.

Taifa Stars leo hii imeambulia kipigo cha mabao 2-0 katika mechi yake ya kirafiki iliyomalizika hivi punde mjini Bujumbura.

Hii ni mara ya pili Stars inafungwa na Warundi hao ambao ndani ya mwezi mmoja tu na ushee, waliifunga Stars mabao 3-0 jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo ya leo , Burundi ilipata mabao yote katika kipindi cha kwanza.
Bao la kwanza lilifungwa na Saido Ntibazonkiza katika dakika ya kwanza tu.

Bao la pili lilifungwa na Yusuf Ndikumana ‘Lule’ katika dakika ya 29.

Source/salehjembe.blogspot.com

Tupia Comments