Michezo

Tanzania inakutana na hawa ili kufuzu World Cup 2018 !

on

tanzania-flagSafari ya kuelekea Kombe la Dunia 2018 Urusi imeshaanza kwa Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA kupanga makundi na ratiba ya michuano hiyo ili kupata timu  zitakazoshiriki fainali hiyo June 2018 Urusi… Droo ya kupanga makundi imefanyika July 25 St Petersburg Urusi.

Taifa-starsKufuatia kupangwa kwa makundi hayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itaanza kucheza hatua ya mtoano na timu ya taifa ya Malawi October 5 2015 kabla ya kucheza mechi ya marudiano October 13 2015.

New+DocumentEndapo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itapita kwa kuifunga Malawi , itakutana na timu ya taifa ya Algeria na mshindi kati yao ataingia hatua ya makundi.

Taifa-Stars (1)Hata hivyo Taifa Stars ambayo inanolewa na Charles Mkwasa chini ya msaidizi wake Hemed Morocco bado ina mechi ya kuwania kufuzu kucheza AFCON 2017 Gabon na timu ya taifa ya Nigeria September 5 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

Taifa-Stars-mazoezini1-620x308Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie

Tupia Comments