Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Wafanyabiashara Liwale watakiwa kujitokeza kupata alama ya ubora (+picha)
Share
Notification Show More
Latest News
Breaking: William Ruto atangazwa kuwa Rais Kenya, Shangwe na furaha zaibuka mitaani Nairobi
August 15, 2022
Matokeo ya Urais Kenya kutangazwa leo, Mgombea Ruto awasili Ukumbini Boma ‘Kusubiria matokeo hayo’
August 15, 2022
Live: Matokeo ya Urais nchini Kenya yanatangazwa muda huu
August 15, 2022
Manara na Wana-Yanga wakomaa kuwa kejeli Simba ‘Mlete Mzunguu’
August 15, 2022
Club ya Wolves ya England kuleta makocha wawili Tanzania
August 15, 2022
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Wafanyabiashara Liwale watakiwa kujitokeza kupata alama ya ubora (+picha)
Top Stories

Wafanyabiashara Liwale watakiwa kujitokeza kupata alama ya ubora (+picha)

August 24, 2021
Share
3 Min Read
SHARE

Wajasiriamli na wenye viwanda Wilayani Liwale mkoani Lindi wametakiwa kujitokeza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa ajili ya kupata alama ya ubora, hatua ambayo itawawezesha kuondokana na vikwazo vya kibiashara na kupanua wigo wa soko la bidhaa zao.

Wito huo umetolewa kwa nyakati tofauti Maofisa wa TBS, wakati walipowatembelea wajasiriamali pamoja na wenye viwanda na kuzungumza nao katika maeneo yao ya biashara kwa lengo la kuwahamasisha wajitokeza TBS kupata alama ya ubora.

Akizungumza na waandishi wa habari Wilayani hapa leo, Afisa Usalama wa Chakula wa TBS, Barnabas Jacob, amesema wapo Wilayani Liwale kwa ajili ya kazi hiyo pamoja na kufanya ukaguzi.

“Kwa hiyo tunatoa wito kwa wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kuthibitisha ubora wa bidhaa zao TBS hatua itakayowezesha bidhaa zao kuondokana na vikwazo vya kibiashara,” Jacob.

Alisema wanachotakiwa kuwa nacho ni barua ya utambulisho kutoka SIDO na baada ya hapo wakifika TBS mchakato unaanza mara moja, hivyo ni muhimu kwao kuchangamkia fursa hiyo.

Jacob alifafanua kwamba alama ya ubora kwa wajasiriamali inatolewa kwao bure na shirika hilo, kwani gharama zote zinalipwa na Serikali, hivyo wanachotakiwa wao ni kupitia SIDO kwa ajili ya kupata barua ya utambulisho.

Pia, Jacob alisema wamefanya ukaguzi wa awali kwa wenye viwanda ambavyo wazalishaji wake wanataka kupata alama ya ubora.

Alitaja miongoni mwa viwanda ambavyo maofisa hao wa TBS wamefanya ukaguzi na kuhamasisha kujitokeza kupata alama ya ubora kuwa ni pamoja na vile vinavyokamua mafuta ya alizeti, viwanda vya kubangua korosho, kwenye mashine za kusaga unga pamoja na kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za mikate.

“Wote hao tumewafikia na kuwahamasisha kuja kupata alama ya ubora TBS” alisema Jacob.

Aidha, alitaja kazi nyingine ambayo wameifanya wilayani humo kuwa ni pamoja na kukagua na kusajili maduka ya vipodozi na chakula ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa kukidhi matakwa ya sheria za nchi na kulinda afya za walaji..

Alisema usajili majengo ya biashara unawapa wafanyabiashara uhakika wa kutunza bidhaa na kwamba wanasajili jengo kulingana na bidhaa zinazoenda kuhifadhiwa humo.

Usajili wa bidhaa, majengo ya vyakula na vipodozi ni takwa la kisheria ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara bila vikwazo.

You Might Also Like

Breaking: William Ruto atangazwa kuwa Rais Kenya, Shangwe na furaha zaibuka mitaani Nairobi

Matokeo ya Urais Kenya kutangazwa leo, Mgombea Ruto awasili Ukumbini Boma ‘Kusubiria matokeo hayo’

Live: Matokeo ya Urais nchini Kenya yanatangazwa muda huu

Azikwa akiwa hai huko Madaba, DC afika eneo la tukio, ‘Jambo hili ni la kinyama’

Rais Samia atoa Bilioni 15 jimboni kwa Shigongo

TAGGED: TZA HABARI
Pascal Mwakyoma TZA August 24, 2021
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Mrembo Gyakie katuletea “Need Me” unaweza kuitazama hapa (Video+)
Next Article Live:Rais Samia ahudhuria uapisho wa Rais wa Zambia
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Breaking: William Ruto atangazwa kuwa Rais Kenya, Shangwe na furaha zaibuka mitaani Nairobi
Top Stories August 15, 2022
Matokeo ya Urais Kenya kutangazwa leo, Mgombea Ruto awasili Ukumbini Boma ‘Kusubiria matokeo hayo’
Top Stories August 15, 2022
Live: Matokeo ya Urais nchini Kenya yanatangazwa muda huu
Top Stories August 15, 2022
Manara na Wana-Yanga wakomaa kuwa kejeli Simba ‘Mlete Mzunguu’
Sports August 15, 2022

You Might also Like

Sports

Club ya Wolves ya England kuleta makocha wawili Tanzania

August 15, 2022
Sports

Inter Milan wawapa Yanga cha kusema, Shaffi Dauda atia neno, Manara apigilia msumari

August 15, 2022
Sports

Barbara awatuliza mashabiki wa Simba, wataka Mzungu aachwe wana mashabiki na mbinu za Kocha

August 15, 2022
Sports

Aziz Ki Mfalme mpya town, mchezo dhidi ya Simba SC ya dhihirissha ubora wake, ‘Jemedari amwagia sifa’

August 14, 2022
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?