Takriban watu 125 wameuawa nchini Msumbiji katika kipindi cha siku tatu za ghasia nchi nzima wakati wa maandamano yaliyoongozwa na upinzani dhidi ya matokeo ya uchaguzi, shirika lislo la kiserikali limesema siku ya Alhamisi
Shirika la Plataforma Decide Alhamis ilitaja idadi ya imefikia 125 tangu Jumatatu, pia kuongeza idadi ya vifo tangu ghasia zilipoanza mwezi Oktoba kufikia 252.
Wakati huo huo huo Kiongozi mkuu wa upinzani wa msumbiji Venansio Mondlane Alhamisi ameshutumu vikosi vya usalama kwa kuchochea ghasia na wizi wa ngawira ili kuruhusu chama tawala kutangaza hali ya dharura baada ya uchaguzi wenye utata.
Mahakama ya juu ya taifa hilo la kusini mwa Afrika ilithibitisha wiki hii kwamba Frelimo kilichopo madarakani tangu kupata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975 kilishinda uchaguzi wa urais uliofanyika Octoba 9 ambao tayari ulisababisha wiki kadhaa za ghasia zilizosababisha mauaji, na kuvunjwa jela ambapo wafungwa takriban 1,000 walitoroka.
Kiongozi wa Frelimo Daniel Chapo alipata asilimia 65.17 ya kura . mpinzani mkubwa wa Chapo, Venansio Mondlane alidai uchaguzi uliibwa na alitangaza kwamba anataka kuchukua Madaraka.
Kiongozi mkuu wa upinzani wa msumbiji Venansio Mondlane leo Alhamisi ameshutumu vikosi vya usalama kwa kuchochea ghasia na wizi wa ngawira ili kuruhusu chama tawala kutangaza hali ya dharura baada ya uchaguzi wenye utata.
Mahakama ya juu ya taifa hilo la kusini mwa Afrika ilithibitisha wiki hii kwamba Frelimo kilichopo madarakani tangu kupata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975 kilishinda uchaguzi wa urais uliofanyika Octoba 9 ambao tayari ulisababisha wiki kadhaa za ghasia zilizosababisha mauaji , na kuvunjwa jela ambapo wafungwa takriban 1,000 walitoroka.