Takriban watu 700 wameuawa nchini Lebanon wiki hii, kulingana na wizara ya afya ya Lebanon, ripoti ya Associated Press (AP).
Israel imeongeza mashambulizi kwa kasi, ikisema inalenga uwezo wa kijeshi wa Hezbollah na makamanda wakuu wa Hezbollah.
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilikadiria kuwa zaidi ya watu 200,000 wamekimbia makazi yao nchini Lebanon tangu Hezbollah ilipoanza kurusha maroketi kaskazini mwa Israel mwezi Oktoba, kuunga mkono Hamas.
Marekani, Ufaransa na washirika wengine kwa pamoja walitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kwa siku 21 ili kujaribu kuepusha vita vya pande zote.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anasema Israel inaishambulia Hezbollah “kwa nguvu kamili” na haitakoma hadi malengo yake yatimie.