Watu 247 wamekamatwa hadi sasa nchini Uturukii kwa amri ya mahakama za nchi hiyo katika mwendelezo wa wimbi la utiaji nguvu wakandarasi wanaoshukiwa kuhusika na ujenzi usiokidhi viwango wa majengo yaliyobomoka katika miji iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi.
Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Uturuki imetaka kuchunguzwa na kuhojiwa wakandarasi na wamiliki wa majengo 997 yaliyoharibiwa na matetemeko mabaya ya ardhi yaliyotokea Februari 6 nchini humo.
Aidha, watu 322 wanaoshukiwa kuhusika na ujenzi usiokidhi viwango wameachiliwa kutoka gerezani kwa masharti ya udhibiti wa mahakama hadi mwisho wa mchakato wa upelelezi wa kesi, huku washukiwa wengine 82 wakiwa wameachiwa huru baada ya kutoa maelezo yaliyohitajika.
mahema takriban laki nne kwa ajili ya kuwapatia hifadhi waathirika wa tetemeko la ardhi katika mikoa 11 ya kusini mwa nchi hiyo na akaongeza kuwa zaidi ya nyumba za muda laki moja pia zimetengwa kwa ajili ya kuwapatia maskani waathirika wa tetemeko hilo la ardhi.
mahema takriban laki nne kwa ajili ya kuwapatia hifadhi waathirika wa tetemeko la ardhi katika mikoa 11 ya kusini mwa nchi hiyo na akaongeza kuwa zaidi ya nyumba za muda laki moja pia zimetengwa kwa ajili ya kuwapatia maskani waathirika wa tetemeko hilo la ardhi. Alisema Murad Korum, Waziri wa Maendeleo ya Miji, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi wa Uturuki.