Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: TAKUKURU yafanya uchunguzi ubadhirifu fedha za hospitali
Share
Notification Show More
Latest News
Jorginho aondoka Chelsea na kusaini Arsenal
February 1, 2023
Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain
January 31, 2023
Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza
January 31, 2023
Waliokutwa na meno ya tembo wahukumiwa miaka 20 jela (+video)
January 31, 2023
Maji ya ajabu yanayotoka bombani Johannesburg
January 31, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Mix > TAKUKURU yafanya uchunguzi ubadhirifu fedha za hospitali
Mix

TAKUKURU yafanya uchunguzi ubadhirifu fedha za hospitali

April 21, 2020
Share
4 Min Read
SHARE

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa  (TAKUKURU)wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro imeanza uchunguzi wa  manunuzi hewa ya vifaa vya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo na ubadhirifu wa fedha zaidi ya shilingi milioni 80(80,000,000),za serikali zilizosababisha kushindwa kukamilisha ujenzi wa majengo mapya saba ya hospitali hiyo ambayo mpaka sasa hayajaanza kufanya kazi kama ilivyotarajiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Siha Deo Mtui alisema  taasisi  hiyo inaendelea na uchunguzi  kwa awamu ya pili katika hospitali hiyo ambapo katika awamu ya kwanza TAKUKURU ilichunguza na kubaini ubadhirifu kwa mzabuni ambae alinunua vitasa duni vya milango hivyo kuamriwa na taasisi hiyo kurudisha fedha zaidi ya  shilingi milioni kumi na moja (Tsh 11,500,000/=) ili iweze kununua vitasa vyenye ubora ambapo alifanikiwa kurejesha fedha hizo.

“Awamu hii Kazi ambayo tunaendelea nayo  ni kwamba tuchunguza zaidi ya shilingi milioni 80 (80,000,000) ambapo katika fedha hizo milioni 80 (Tsh 80,000,000/=) tunachunguza fedha kiasi cha shilingi 16,000,000 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kulipa mafundi na kiasi cha shilingi  27,000,000/= ambazo zilitumika kufanya malipo hewa ya vifaa hewa na kiasi cha shilingi 30,000,000/= tunazoendelea kuchunguza ni fedha ambazo zimetumika kizembe kununua vifaa vingi ambavyo vilikuwa havihitajiki.”>>> Mtui 

Mkuu wa wilaya hiyo Onesmo Buswelo akizungumzia sakata hilo alisema kama pamoja na kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa kiasi cha shilingi  1,500,000,000/=  kwa ajili ya kujenga majengo mapya ya hospitali ya wilaya walikumbana na changamoto kadhaa ambazo baada ya majengo hayo kutokamilika kwa wakati jambo ambalo walitilia shaka uadilifu na uaminifu wa baadhi ya watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia ujenzi huo.

Alisema walipata mashaka kwenye maeneo ya uagizaji wa vifaa, upokeaji na kwenye malipo jambo ambalo lilisababisha kamati ya usalama wilaya ya Siha kuelekeza  TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina lakini pia kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndaki Mhuli kupitia mkaguzi wa ndani kufanya uchunguzi kuona ni wapi fedha hizo zimeishia.

“Katika fedha hizo tulitarajia ibaki kiasi cha shilingi milioni mia moja kumi na nane (118,000,000) kwa ajilia ya njia za kwenda kwamiguu hospitalini hapo lakini cha ajabu ilipofika januari mwaka huu  mkurugenzi alisema hana fedha na kazi haijaisha hivyo uchunguzi wa awali ulibaini kuwa kulikuwa na udanganyifu kwa mhandisi pamoja na timu yake.”>>> Buswelo

Alisema katika uchunguzi wa awali ilionesha kuwa mhandisi na timu yake walifanya udanganyifu wa fedha zote walizotakiwa kulipa mafundi na katika kuwalipa zilibaki zaidi ya shilingi milioni kumi na saba (17,000,000) ambazo hazijulikani zilipo huku zikionesha zipo ofisi ya mhasibu ambako napo hazipo.

“Sasa mapungufu hayo  pamoja na mengine na ubadhirifu huu tumewapa kazi TAKUKURU na mimi mwenyewe kwa mkono wangu niliwaandikia barua kuwataka kufanya uchunguzi mapema itakavyowezekana na kisha hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wahusika kwa kuwa unataka fedha ya umma ifanye kazi kama ilivyokusudiwa ili itupatie matokeo chanya kama ambayo mhe Rais na watanzania wanavyotazamia.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmasahuri ya Siha Ndaki Stephano Mhuli alisema kama halmashauri kwa nafasi yao wamechukua hatua kwa wahusika wote na wameunda kamati ya uchunguzi kwa maana ya taratibu za kinidhamu ili kubaini makosa ya wahusika.

Hata hivyo kwa mujibu wa maagizo ya Serikali hospitali zote 67 za wilaya ambazo zilipewa fedha na serikali kiasi cha shilingi bilioni 1.5 zilipaswa kuwa zimekamilika na kuanza kazi ifikapo Machi mosi 2020 agizo ambalo kwa wilaya ya Siha limeshindwa kutekelezwa kutokana na ubadhirifu huo.

VIDEO: VITA DHIDI YA CORONA, BARAKOA MILIONI TATU KUZALISHWA NCHINI

You Might Also Like

Fredy Lowassa akabidhi vifaa vya shule kwa waliofauli 2023

Gynah ni mwimbaji wa kimataifa kenye usiku wa Kahawa

PICHA: Jerry Muro akabidhi madarasa 29 kwa RC Singida

Samsung wafungua duka lao ndani ya Palm village Mikocheni

Hatimaye Miss Tanzania 2020 akabidhiwa zawadi yake

TAGGED: habaridaily
Rama Mwelondo TZA April 21, 2020
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo April 21, 2020
Next Article CORONA: Marekani bei ya mafuta yashuka chini ya Dola 0
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Jorginho aondoka Chelsea na kusaini Arsenal
Sports February 1, 2023
Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain
Top Stories January 31, 2023
Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza
Top Stories January 31, 2023
Waliokutwa na meno ya tembo wahukumiwa miaka 20 jela (+video)
Top Stories January 31, 2023

You Might also Like

Top Stories

Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain

January 31, 2023
Top Stories

Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza

January 31, 2023
Top Stories

Maji ya ajabu yanayotoka bombani Johannesburg

January 31, 2023
Top Stories

Biden akataa kutuma ndege za kivita Ukraine

January 31, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?