Ni Mkali kutokea Bongoflevani, Billnas ambae tangu aachie collabo yake mpya aliyomshirikisha Jay Melody inaendelea kufanya vizuri kwenye platfoms mbalimbali.
Na Mpaka sasa wimbo huo kupitia Shazam umeweza kutafutwa na watu wasiopungua 50,000 (Ukishika Namba moja kwenye Chat ya Shazam Tanzania na Kenya) na Kupitia mtandao wa Tiktok wimbo huo umetumika kama kionjo kwa watu zaidi ya 300k huku kupitia platforms mbali mbali duniani ukiwa na total stream Milioni 5 tangu ulipoachiwa Desemba 9, 2022.
Huku mtandao Boomplay ukiwa unaongoza collabo hii imesikilizwa na watu zaidi ya Milioni 3.4 ukifuatiwa na mtandao wa Youtube 800k views.
Takwimu hizo zimetolewa na Kampuni ya Usambazaji na usimamizi wa kazi za wasanii maarufu kama Slide Digital.