Habari za Mastaa

“Tale alitakiwa kunipenda…nilikuwa msanii mkubwa kabla yake” – Chid Benz

on

Leo June 22, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM rapa mkongwe Bongo Chid Benzi amefunguka na kueleza kilichotokea kipindi ambacho Babu Tale alijitolea kumsaidia ili arudi kwenye hali ya zamani na kuendelea na maisha yake kama awali.

Chid Benzi amesema kuwa Babu Tale angemvumilia na hali yake aliyokuwa nayo kabla ya kukata tamaa ingawa anampenda na kumuheshimu kama kaka yake na hana maana kuwa alikosea kumuacha kipindi kile.

>>>“Nilikuwa na game yangu kitambo na Tale alitakiwa kunipenda. Angevumilia tu maana nilikuwa msanii mkubwa kabla yake kwenye game. Kipindi nipo zangu Sober ilikuja list ya Magezeti wapo watu wanavuta Unga, niligundua tupo wengi kumbe sipo peke yangu.

“Tale asinitangaze kwenye Media mimi nimerudia Madawa, yeye ni kaka yangu napenda tuishi kama ndugu siku zote. Sikuwepo Wasafi, nilienda pale kama La Familia ila Tale alikuwa ananisimamia kama mdogo wake tu. Nahangaika sana kupambana ili nitoke kwenye hili janga, now am okay.” – Chid Benzi.

Kitu Amini anatamani Rais Magufuli afanye kwenye Bongofleva!!!!

EXCLUSIVE: “Nimeingia rasmi kwenye Ubondia” – Yusuph Mlela

Soma na hizi

Tupia Comments