fB insta twitter

Maneno ya Babu Tale kwa DJ Choka baada ya kuweka wazi kuwa aliugua TB

By

on

Meneja wa kundi la Tip Top Connection pamoja na mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz, Babu Tale ameizungumzia issue ya DJ Choka kuweka wazi kuwahi kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) mpaka alivyopata matibabu na kupona.

Babu Tale alitumia ukurasa wake wa Instagram kumpongeza DJ Choka kwa kuamua kuweka wazi alichokuwa anaumwa akisema ni mfano wa kuigwa kwani watu wengi wamekuwa wanaficha juu ya magonjwa yanayowakibili.

“Wahenga walisema mficha uchi hazai, wakazidi kusema mficha maradhi kifo humuumbua, kwanza kabisa nimeguswa na kufurahishwa na kitendo cha kijasiri alicho kifanya ndugu yangu @chokadj kwa kuiwekea wazi jamii nini alikwa anaumwa na kwa kudra zake Mungu akapona.

“Imekuwa ni jadi sikuhizi kwa vijana wengi alwatan kuficha maradhi yao huku wakisahau hofu na wasiwasi pia nayo ni ugonjwa, na kadri unavo zidi kuficha ndivyo kadri ugonjwa unazidi kukomaa.

@chokadj kawa mfano mzuri kwa jamii yetu ya sasa kudhihirisha kuwa kuficha maradhi si suluhisho wa tiba ya ugonjwa wako, ni wangapi jana walikuwa wamejifungia ndani wakiugulia TB huku mioyo yao ikiamini TB haitibiki lakini baada ya @chokadj kujitokeza na kuiambia jamii ameuguwa ugonjwa huo na kupona leo wagonjwa hao hao wapo kwenye foleni hospitalini wakingojea huduma ya matibabu.

Ndugu zangu halimpati mtu jambo isipo kuwa Mungu kutaka kwan kwa hakika ni yeye pekee atupae mitihani na majibu yake akakupatia. Sasa nazidi kuaminu TB ina tibika. #AsanteChoka Babu Tale.

Wahenga walisema mficha uchi hazai, wakazidi kusema mficha maradhi kifo humuumbua, kwanza kabisa nimeguswa na kufurahishwa na kitendo cha kijasiri alicho kifanya ndugu yangu @chokadj kwa kuiwekea wazi jamii nini alikwa anaumwa na kwa kudra zake Mungu akapona. Imekuwa ni jadi sikuhizi kwa vijana wengi alwatan kuficha maradhi yao huku wakisahau hofu na wasiwasi pia nayo ni ugonjwa, na kadri unavo zidi kuficha ndivyo kadri ugonjwa unazidi kukomaa. @chokadj kawa mfano mzuri kwa jamii yetu ya sasa kudhihirisha kuwa kuficha maradhi si suluhisho wa tiba ya ugonjwa wako, ni wangapi jana walikuwa wamejifungia ndani wakiugulia TB huku mioyo yao ikiamini TB haitibiki lakini baada ya @chokadj kujitokeza na kuiambia jamii ameuguwa ugonjwa huo na kupona leo wagonjwa hao hao wapo kwenye foleni hospitalini wakingojea huduma ya matibabu. Ndugu zangu halimpati mtu jambo isipo kuwa Mungu kutaka kwan kwa hakika ni yeye pekee atupae mitihani na majibu yake akakupatia. Sasa nazidi kuaminu TB ina tibika. #AsanteChoka

A post shared by Hamisi Taletale (@babutale) on

Soma na hizi

Tupia Comments