Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

Habari za Mastaa

Meneja Babu Tale imebidi ayaseme haya kuhusu kauli ya Diamond kupitisha video MTV BASE

on

Hii ni stori ambayo ilianza kuandikwa wiki iliyopita baada ya Diamond kufanya interview na TBC Fm kwenye kipindi cha Papaso ambapo miongoni mwa maswali aliyoulizwa ni namna ipi anawasaidia wasanii wa Tanzania baada ya kusemekana yeye anawabania nje ya nchi.

Jibu alilolitoa Diamond alisema kuwa hawabanii Watanzania wenzake na ndiyo sababu hata video za wasanii wa Tanzania zinapofika kwenye kituo cha MTV hupigiwa simu na kuulizwa, kauli hii imeleta utata kiasi kwamba Uongozi wa Diamond umeamua kuutolea ufafanuzi.

Babu Tale alihojiwa na XXL ya Clouds Fm na kusema >>> ‘Ingekua ni kweli…. wimbo wa Harmonize ambaye ni msanii wa Diamondi ingekua inapigwa kila siku au ingekua Exclusive MTV sababu ndio biashara yake, hilo sio neno la ukweli… yule aliyeitoa hiyo habari amekichukua kichwa cha habari na kukifanya habari kwa watu wengine’

‘Diamond aliulizwa Wasanii gani ambao amewasaidia na anasupport vipi muziki wa nyumbani kwenda nje, akajibu mimi mbona huwa nasaidia watu wengi? na kuna kipindi mtu huwa ananipigia simu kuuliza unamjua flani? ni mzuri? kuna media za nje huwa zinanipigia kuuliza kama namjua flani? hivyo tu na yeye huwa anasema mzuri ili Watanzania wapae‘ – Babu Tale

Kwa kumalizia, Tale amesema ‘Aliyeandika kile kichwa cha habari akasema DIAMOND NDIYE ANAAMUA MTU FLANI KUCHEZWA SEHEMU TV FLANI, sio kweli… kama Diamond angekua anaamua hivyo basi nyimbo zote za TMK, Mkubwa na wanae na wote wa karibu na Diamond zingekua zinapigwa sana MTV

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments