Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji mkoani Pwani Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa leo ameshiriki dua maalum ya kumuombea aliyekuwa Mwanasiasa mashuhuri kwenye historia ya Tanganyika na harakati za ukombozi wa bara la Afrika marehemu Bibi Titi Mohamed shughuli iliyofuatiwa na uzinduiz wa Tamasha la kumbukizi ya Bibi Titi (Bibi Titi Memorial Festival 2023)
Shughuli imefanyika nyumbani kwa kwa Mtoto pekee wa Marehemu bibi Titi Mohamed, Bi Halima Mzee.
@mrishompoto ni miongoni mwa watu mashuhuri walioshiriki shughuli hiyo.
Imeelezwa kuwa kutakuwa na mbio maalum za ushindi kutoka DSM hadi Rufiji mahali ambapo tamasha hili hufanyika.