Mamilioni ya watu wanahudhuria tamasha la Kihindu la Kumbh Mela – linalofafanuliwa kama mkusanyiko mkubwa zaidi wa watu – katika jiji la Prayagraj kaskazini mwa India siku ya Jumatatu.
Tukio hilo – linalofanyika mara moja kila baada ya miaka 12 – linaanza Jumatatu na kuendelea kwa zaidi ya wiki sita zijazo, wacha Mungu wataoga huko Sangam – katika mto mtakatifu zaidi wa Ganges wa India na mto wa Yamuna na Saraswati ya kufikirika.
Wahindu wanaamini kwamba kuoga katika mto mtakatifu kutawaondolea dhambi, kutakasa roho zao na kuwakomboa kutoka kwa mzunguko wa kuzaliwa na kifo – kwani lengo kuu la Uhindu ni wokovu.
Takriban mahujaji milioni 400 wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hilo la siku 45, ambalo ni kubwa kiasi cha kuweza kuonekana kutoka angani.
Leo Jumatatu, waumini milioni tano hadi nane wataoga huku siku inayofuata, idadi hiyo ikitarajiwa kuzidi milioni 20.
Tamasha la Jumanne litakuwa la kipekee kwani litawashuhudia watakatifu wa Kihindu waliopakwa majivu wakiwa na vazi la nywele zilizochanika, wanaojulikana kama Naga sadhus, wakijizamisha ndani ya maji na baadaye kutoka katika jiji la kaskazini mwa India alfajiri.
Lakini mamlaka hazijitayarisha kikamilifu kuwakaribisha mamilioni ambao wataendelea kumiminika katika tamasha hilo.