Mix

Tamthilia ya The Queen Of Flow ilishinda tuzo za Emmy sasa inaanza kuonekana Tanzania

on

Tanzania sasa inapewa fursa nyingine ya kuona tamthiliya ya The Queen Of Flow baada ya kuwa na mafanikio makubwa na kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo za Emmy ambazo hutolewa nchini Colombia.

Tamthiliya hii mvuto wake unatajwa ni kutokana na umahiri ya waigizaji waliocheza, tamthiliya hii sehemu  kidogo inamuhusisha binti aliyekuwa mahiri katika sanaa ya muziki ambaye anasalitiwa na mpenzi wake na kumfanya aende jela, baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 jela binti anarejea uraiani akiwa na umri wa miaka 34.

Binti karejea uraiani na utambulisho mpya kwa lengo la kutaka kulipa kisasi kwa wale wote waliopanga njama za kutaka ahukumiwe ikiwemo aliyekuwa mpenzi wake, afisa masoko wa Star Times David Malisa amethibitisha kuwa tamthiliya hii watanzania wataiona kuanzia December 15 2019 kupitia ST Novela hii kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

VIDEO: Muhitimu wa Chuo Kikuu aliyebuni mashine ya kuparua na kusafisha samaki kwa sekunde 5

Soma na hizi

Tupia Comments