Licha ya TANESCO kutangaza mgao wa umeme wa siku kumi kuanzia tarehe 1 mpaka 10 February 2022 kutokana na marekebisho katika bomba la kuingiza gesi, Mkurugenzi wa Shirika hilo Maharage Chande amesema hata hivyo mgao huo sio wa Nchi nzima.
Akizungumza Jijini Dar es salaam leo baada ya kutembelea mradi wa kutembelea umeme kwa kutumia gesi wa Kinyerezi II amesema “Ili gesi ipatikane kwa wingi kwenye hii mitambo mipya wamepanga kufanya maboresho haya kuanzia February 1-10 hivyo wakiwa wanafanya maboresho haya watazima mitambo mingine kupisha uboreshaji ufanyike”
“Kwa sababu hiyo kuna maeneo yatakuwa na upungufu wa umeme lakini sio Nchi nzima lakini kutakua na athari kwenye baadhi ya maeneo na tutatoa ratiba kuanzia kesho mpaka tarehe 10 kuhusu wapi pataathirika ili Wananchi na Viwanda waweze kujipanga” ——— Maharage Chande.