Mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Tanga Ramadhani Omary amewataka vijana Mkoani Tanga kutoshiriki kwenye swala zima la Usafirishaji wa Wahamiaji haramu kwani kufanya hivyo ni kukiuka Sheria za nchi.
Ramadhani ameyasema hayo Wilayani Handeni wakati akizungumza na vijana wa boda boda na wanachama wa CCM Wilayani humo.
Ikiwa ni maadhimisho ya kuelekea miaka 46 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM na kusema kuwa kuendelea na kushiriki kwa Vijana kwenye usafirishaji wa Wahamiaji ni kupelekea kuhatarisha nchini yetu hivyo ni Muhimu kushiriana na Jeshi la Polisi kufichua wahalifu wanao fanya vitendo hivyo.
“Sisi kama umoja wa vijana hatuwezi kuwa ndo sababu ya kusafirisha wahamiaji haramu hivyo kwani kipato ambacho tunakipata kwa kusafirisha wahamiaji haramu kinaweza kupeleke uhalifu kwenye maeneo yetu “Alisema Ramadhani..
Aidha mwenyekiti huyo wa vijana Mkoa wa Tanga ametoa rai kwa Vijana wanaopata nafasi ya kupata mikopo ya asilimia kumi kutoka Halmashauri wawe na taratibu ya kurudisha ili kuwawezesha na wenzao kuweza kukopesheka.
“Kwakweli inasikitisha sana kuona serikali yetu inawawezesha mikopo vijana isio na riba lakini vijana hao hao ndo wamekuwa kikwazo cha kurudisha mikopo hiyo hilo sio jambo zuri nasio dhamira ya serikali yetu “– Alisema Ramadhani
Hata hivyo mwenyekiti huo amefanikiwa kugawa kadi za umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi CCM kwa wanachama wapya zaidi ya miamoja Wilayani handeni Mkoani Tanga.