AyoTV

VIDEO: Watu watano waliokamatwa na Polisi Dodoma

on

Taarifa kutokea Jeshi la Polisi Dodoma May 6, 2017 ni kuhusu matukio mawili tofauti yaliyofanyika mkoani hapo yakihusisha kukamwatwa kwa watuhumiwa watano huku wanne kati yao wakihusika na matukio ya ujambazi.

Kamanda wa Polisi Dodoma Lazaro Mambosasa amesema…>>>’Katika tukio la kwanza Polisi inamshikilia Jumaa Ndosa mkulima wa Gairo, Morogoro aliyekamatwa akiwa na gunia moja la mirungi lenye uzito wa kilo 50 alizokuwa akisafirisha kwa kutumia pikipiki

Tukio la pili Polisi katika uchunguzi uliofanywa na Polisi katika kijiji cha Kibakwe Wilaya ya Mpwapwa katika nyumba ya Msafiri Philipo na Frank Mapembe tulifanikiwa silaha tatu aina ya Gobore na risasi aina ya chuma 70 zilizokuwa zikitumika kinyume cha sheria‘- Lazaro Mambosasa

VIDEO: Waziri mkuu anunua hisa za Vodacom 

Soma na hizi

Tupia Comments