Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Wakala ya Barabara (TANROADS) imechukua jitihada za makusudi na haraka kuhakikikisha inarejesha mawasiliano ya barabara ya Ibungu hadi Kafwafwa, sehemu za vijiji vya Sange, Kawalisi, Ruswisi iliyojifunga kwa muda wa takribani masaa matatu kutokana maporomoko ya ardhi (landslide) yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Ireje na mkoa wa Songwe kwa ujumla.
TANROADS mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa na Wilaya waliweza kurejesha mawasilino ya barabara hiyo ndani ya muda mfupi na kurejesha matumaini na furaha kwa watumiaji wa barabara hiyo muhimu kuunganisha mkoa wa Songwe kwa wilaya ya Ileje na Mkoa jirani wa Mbeya kwa wilaya ya Rungwe.Aidha, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha TANROADS wameweka kambi maeneo mbalimbali katika Wilaya za Momba, Mbozi, Songwe na Ileje kuhakikisha miundombinu inapitika bila shida.
Wananchi wanaotumia barabara ya Ibungu hadi Kafwafwa wamepongeza Serikali na kipekee Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) Waziri wa Ujenzi kwa namna miundombinu inavyoshughulikiwa wakati huu wa mvua za Elnino Zinazoendelea nchini Ofisi ya Meneja wa Mkoa TANROADS imewasihi na kuwaomba Wananchi mara wanapopata changamoto za barabara wasisite kutoa taarifa kwa viongozi ili taarifa zifike kwa wakati ili kurahisisha kurejesha mawasiliano ya barabara. Aidha Meneja wa Mkoa TANROADS Eng Suleiman Bishanga amewashukuru wananchi wa Wilaya ya Ireje kwa kufikisha taarifa mapema na changamoto hiyo imetatuliwa mapema.