Ni uzinduzi wa Tuzo za wachekeshaji nchini TCA ambao umezinduliwa Usiku huku ukiwa na usimamizi wa baraza la Sanaa la Taifa BASATA na Bodi ya filamu chini ya Wizara ya Utamaduni, sanaa na Michezo ikisimamiwa na Naibu waziri wa wizara hiyo Khamisi Mwinjuma
Tuzo za TCA ( Tanzania Comedy Awards ) zina category 21 na zinatarajiwa kutolewa mwezi February tarehe 14 katika Ukumbi wa the Super Dom Masaki ukiwahusisha wachekeshaji wote nchini na washindi wa Tuzo kumbwa tatu za juu watapokea na pesa kwa mchanganuo ufuatavyo Mchekeshaji bora Wakike Milioni 20, Mchekeshaji bora Wakiume Milioni 20, na Mchekeshaji bora wa Mwaka wa jumla Milioni 30, Huku washindi wa Tuzo wengine watapata Milioni 5 kila mshindi wa Tuzo.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa Tuzo za wachekeshaji wote zilizopo chini ya Serikali na katika Uzinduzi huu wamehudhuria wachekeshaji wakongwe na wapya akiwemo Bambo, Kingwendu, Joti, Mtanga na wengine wapya..