Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) imesema kwa sasa Tanzania ina uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati 5000 za umeme (MWe) zitokanazo na jotoardhi.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 23, 2021 jijini Dar es Salaam na Meneja Mkuu na Mtendaji Mkuu wa TGDC, Kato Kabaka wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara.
Amesema jotoardhi hilo ambalo linatokana na joto la asili la dunia lililopo chini ya ardhi katika mfumo wa majimoto, mvuke au miamba mikavu linapatikana katika mikoa zaidi ya 16 ya Tanzania bara.
Kabaka amesema maeneo hayo yapo katika sehemu zilizopitiwa na Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki na Magharibi na kuongeza kuwa kulingana na mpango wa Taifa wa uzalishaji umeme wa mwaka 2020 wanalengo la kuzalisha Megawati 200 na 500 za joto zitokanazo na jotoardhi ifikapo mwaka 2025.
“Mafunzo ya jotoardhi hayatolewi na vyuo vya ndani ya nchi bali utolewa na vyuo vya nje, mpaka sasa tumewezesha wataalamu hao kwenda kusoma na wengine bado wapo nje ya nchi wakikamlisha kozi zao,” Kabaka
“Lengo la miradi hii ni kuonesha jinsi rasilimali ya jotoardhi inavyoweza kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za uchumi na kutoa fursa za ajira mpya kwa vijana,” Kabaka