Tanzania imeibuka kati ya washindi kwenye Shindano la Shirikisho la Kimataifa Mchezo wa Ndege Kipanga (International Federation for Falconry Sports and Racing Cup UAE) lililofanyika Dubai, Falme za Kiarabu (UAE). Katika mashindano hayo Tanzania iliwakilishwa na Akram Azizi ambaye aliingoza timu Kilombero North Safaris Limited (KNSL).
Shindano hilo limefanyika Dubai kwa mwaka wa pili mfululizo ambapo mwaka huu limeshirikisha timu 23 toka mataifa 21, likiwa limeasisiwa na Sheikh Ahmed bin Mohammed bin Rashid Al Maktoum ambaye ni Makamu Mtawawala wa Dubai na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo.