Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania yang’ara mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu Afrika
Share
Notification Show More
Latest News
Jorginho aondoka Chelsea na kusaini Arsenal
February 1, 2023
Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain
January 31, 2023
Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza
January 31, 2023
Waliokutwa na meno ya tembo wahukumiwa miaka 20 jela (+video)
January 31, 2023
Maji ya ajabu yanayotoka bombani Johannesburg
January 31, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Sports > Tanzania yang’ara mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu Afrika
Sports

Tanzania yang’ara mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu Afrika

November 28, 2022
Share
3 Min Read
SHARE

Waogeleaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ya wanaume na wanawake (Tanzanite) wameipeperusha vyema bendera ya nchi baada ya kushinda mashindano ya Kanda ya tatu Afrika yaliyofanyika hivi kariibuni kwenye bwawa la klabu ya Dar es Salaam Gymkhana.

Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha jumla ya nchi 10, waogeleaji wa Tanzania walikusanya jumla ya pointi 3,061 na kuzishinda nchi tisa katika mashindano hayo yaliyokuwa na ushindani mkubwa na kusisimua.

Tanzania ambayo iliwakilishwa na waogeleaji 63 pia ilikuwa nchi pekee iliyoshinda medali nyingi kushinda nchi zote zilizoshiriki katika mashindano hayo. Tanzania ilishinda jumla ya medali 110.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na chama cha mchezo huo cha kanda ya tatu Afrika, nafasi ya pili ilikwenda kwa Kenya ambayo ilijikusanyia pointi 2,768 na kufuatiwa na Uganda iliyojikusanyia pointi 2,521.50 na Zambia katika nafasi ya nne kwa kukusanya pointi 1,878.

Afrika Kusini ilishinda nafasi ya tano kwa kupata pointi 1,385. 50 ambapo Burundi  ilishika nafasi ya sita kwa kupata pointi 653  na Sudan Kusini ikimaliza katika nafasi ya saba kwa kupata pointi 213.

Nchi za Djibouti ( pointi 87), Rwanda (pointi 67) na Ethiopia iliyopata pointi 47 zilimaliza katika nafasi ya nane, tisa na 10 katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa naKilombero Sugar Company  kupitia Bwana Sukari.

Wadhamini wengine ni JustFit, Kahawa Café, Spark rehabilitation, Gymkhana Club, International School of Tanganyika, FK International school, Hopac Hawks, Pepsi, Travelport, Azam, Stanmag Logistics, Wood Lab Décor, Burger 53, F&L Juice, G1 Security, Leo Club of Tanzania District 411C, Suraksha Team, Pyramid consumers, Four Points by  Sheraron, Crown Hotel, Aura Suites na Protea Hotel Mariot- Courtyard.

Kwa upande wa medali, Tanzanian ilikusanya jumla ya medali za dhahabu 38,  Fedha 38 na Shaba 34 ikifuatiwa na Kenya ambayo ilipata jumla ya medali 108 ambapo 46 ni dhahabu, Fedha 32 na Shaba 30.

Uganda ilipata jumla ya medali 85  ambapo 28 zilikuwa za dhahabu, 25 fedha na shaba 32 na Zambia ilipata jumla ya medali 56, 22 (dhahabu), 21 (fedha) na 13 shaba.

Afrika Kusini ilipata jumla ya medali 30 ambapo nane (8) ni dhahabu, nane za fedha na 14 za shaba. Nchi za Burundi, Sudan na Rwanda zilishika nafasi ya sita, saba na nane kwa kukusanua jumla ya medali 20, 10 na tatu (3) huku nchi za Ethiopia, Djibouti na Sudani Kusini zikiambulia patupu.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Hadija Shebe aliwapongeza waogeleaji na timu zote shiriki kwa kufanikisha na Tanzania kuibuka washindi kwa mara ya tatu katika historia. Tanzania mara ya kwanza ilishinda taji hilo mwaka 2016 mjini Kigali, Rwanda na mwaka uliofuatia katika mashindano yaliyofanyika hapa nchini.

Shebe pia aliwapongeza wajumbe wa kamatiya maandalizi ya mashindanin hayo ambao ni Bella Faya, Geetha Prashant, Priscilla Zengeni, Lingesh Ramasamy, Martha Makoi, Opalina Nanyaro, Tunu Kinabo, Joan Laiser na Francisca Binamungu.

You Might Also Like

Jorginho aondoka Chelsea na kusaini Arsenal

Jorginho yametimia Arsenal

Picha: Tazama wadau mbalimbali waliohudhuria kushuhudia mkataba wa Yanga na Haier

Live: Yanga SC yaingia mkataba na kampuni ya Haier wenye thamani ya Bilioni 1.5

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Simba SC, Mangungu minne tena

TAGGED: Sports
Rama Mwelondo TZA November 28, 2022
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Mchimba madini akamatwa kwa mauaji
Next Article Upatikanaji maji DSM Asilimia 100
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Jorginho aondoka Chelsea na kusaini Arsenal
Sports February 1, 2023
Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain
Top Stories January 31, 2023
Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza
Top Stories January 31, 2023
Waliokutwa na meno ya tembo wahukumiwa miaka 20 jela (+video)
Top Stories January 31, 2023

You Might also Like

Top Stories

Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain

January 31, 2023
Top Stories

Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza

January 31, 2023
Top Stories

Maji ya ajabu yanayotoka bombani Johannesburg

January 31, 2023
Top Stories

Biden akataa kutuma ndege za kivita Ukraine

January 31, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?