Serikali ya Marekani imepiga marufuku Raia wa Tanzania kushiriki katika Bahati Nasibu ya kupata Viza (Visa) ya kuingia Marekani, hatua iliyotangazwa saa chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kuzuiwa kuingia nchini Marekani.
Bahati Nasibu hiyo hutoa Viza kwa watu takriban 50,000 kutoka nchi zenye kasi ndogo ya maendeleo kila mwaka kuingia na kufanya kazi Marekani.
Aidha, Raia wa Sudan pia wamepigwa marufuku kuingia katika Bahati Nasibu hiyo huku Raia wa nchi nne ambazo ni Kyryzstan, Myanmar, Nigeria na Eritrea wamepigwa marufuku kabisa kuomba Viza za kuhamia Marekani.
Hata hivyo Raia wa nchi hizo ambao watataka kuingia Marekani kwa kutalii ama biashara wataruhusiwa.