Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava amewataka wakala wa barabara vijijini na mijini TARURA mkoa wa Morogoro kuendelea kuboresha miundo mbinu ya usafiri na usafirishaji kwa kujenga barabara kwa ubora na viwango ili ziweze kutumika kwa muda mrefu bila kiharibika.
Aidha Mnzava alisema kuwa baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo mwenge wa uhuru umeridhishwa na mradi wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha zege ya kichangani iliyopo kata ya mji mpya manispaa ya morogoro.
Hata hivyo kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 0.45 alisema kuwa tarura wamefanya kazi nzuri ambayo inaonekana na inafanana na fedha iliyotumika.
Pia kiongozi wa mbio za mwenge baada ya kupima na kujiridhisha na barabara hiyo alisisitiza kutunzwa kwa barabara hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu.
Kwa upande wake meneja wa TARURA manispaa ya Morogoro mhandisi Mohamed Muanda alisema kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 0.45 sawa na mita 450 za barabara ya kiwango cha zege ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 63, ukigharimu milioni 470 , ina imuhimu mkubwa sana katika kuleta uchumi wa wakazi wa eneo husika.
Naye meneja wa TARURA mkoa wa Morogoro mhandisi EMMANUELNDYAMUKAMA alisema amepokea maelekezo ys kiongozi wa mbio za mwenge na watazingatia maelekezo hayo ili kuendelea kiboresha na kujenga kwa viwango barabara na kuinua uchumi wa wa wananchi wa mkoa wa morogoro.
Mbunge wa Morogoro mjini na diwani wa kata ya mji mpya Emmy Kiula wakapongeza ujenzi huo na kusema awali barabara hiyo imejengwa mara mbili kwa kiwango cha lami na kubomoka kutokana na kiwango cha maji kuwa juu hivyo kusindwa kudumu kwa kipindi kirefu.
hata hivyo sambamba na hayo diwani Emmy Kiula aliomba barabara hiyo kueekwa taa za barabarani ili kusaidia uzalishaji wa mashine za kusaga nafaka na viwanda vingine viweze kufanya kazi hadi usiku.