Shirika la uwakala wa meli Tanzania TASAC limewaomba wamiliki wote wa vyombo vya usafiri Majini kuvitumia vyombo hivyo kama vilivyosajiliwa kutumika na si vingine na hatua za kisheria kwa mmiliki yoyote atayekitumia chombo hicho kunyume zitachukuliwa
Akifafanua namna TASAC inavyofanya kazi kuthibiti ajali sambamba na kutoa elimu ya kujikinga Afisa Masoko Mwandamizi shirika la uwakala wa meli Tanzania Tasac Martha kelvini amesema TASAC inafanya ufatiliaji na ziara za kustukiza Mara kwa Mara kwenye maeneo ya ziwa kuangali kama vyombo hivyo vinatumika kama vilivyopangwa
Aidha kwa upande Afisa uthibiti huduma ya bandari Victoria Miyonga amesema jukumu la tasac ni kuhakikisha vyombo vya usafiri Majini viko na ubora sambamba kuwa vitu vya kujikuoa kipindi panapotokea ajali
Sambamba na hayo maonyesho ya Madini yamesaidia kupeleka elimu kwa wananchi kujua namna ya kujikinga na ajali za Majini ambapo wananchi wametembelea banda hilo na kujifunza mambo mbalimbali.