Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa taarifa kuhusu tukio la kuzama kwa boti ya uvuvi ya MV LEGACY na kusema kuwa ilizama ikiwa katika majaribio ya kiufundi baada ya matengenezo ya mifumo ya uvuaji samaki kwa kukokota.
Taarifa ya TASAC iliyotolewa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa boti hiyo illyozama Machi 10, 2024 majira ya alasiri ilianza majaribio majira ya saa tatu asubuhi ikitokea maeneo ya Tandavamba, Kivukoni na kufanya majaribio ya kuvua samaki kuzunguka katika maeneo yenye maji mafupi karibu na eneo la daraja jipya la Tanzanite hadi Coco Beach.