Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani amesema kuwa katika Jiji la Tanga, tatizo la ajira kwa vijana ni changamoto inayolikabili hivyo hawana budi kupambana nayo kwa nguvu zote kwa kushirikisha Serikali na wadau wengine wa maendeleo kama botna foundation.
Amesema kuwa kulingana na sensa ya Takwimu ya Taifa (NBS), bado changamoto ya ajira kwa vijana ni kubwa na kila mmoja anahitajika kuchukua hatua wakiwemo vijana wenyewe kwa kutafuta ajira na kujiajiri.
Amesema takwimu hizo za NBS, zinaonyesha kuwa vijana 147,000 wenye umri wa miaka 15-35 katika jiji hilo 109,000 wameajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi,
“Lakini wapo takribani 5,000 wanatafuta kazi kwa sasa. Inasikitisha sana kuona kuwa kuna vijana takriban 30,000 hawatafuti kazi na wala hawataki kusoma.
Hili ni tatizo la kijamii na nilazima tushirikiane kulitatua,”
Kwa upande wa Botna foundation kupitia kwa Hassan Mshinda amesema kuwa mradi wa pili wa Tanga yetu utagharimu kiasi Cha shilingi Bil.8 huku akiwasihi vijana kuchangamkia fursa za uvuvi,Elimu,Afya na kilimo.