Mix

Umesikia story ya uwanja wa ndege kupata tatizo la IT? Isome hapa.

on

ITImetokea mara nyingi kusikia Watanzania wakilalamika masuala mbali mbali, mfano ni huu. Unakumbuka ni mara ngapi unahitaji kutoa pesa ATM na ukakuta haiifanyi kazi kutokana na tatizo la Network? Au unakumbuka ni mara ngapi unapiga simu halafu unajibiwa namba haipatikani?

Sasa story ni kwamba hayo mambo ya ‘system failure’ au matatizo ya mtandao hata Ulaya yapo, headline kutoka Uingereza inasema wafanyakazi katika uwanja wa ndege ambao uko busy zaidi Uingereza wa Heathrow, walijikuta na jukumu la kubeba mizigo ya abiria kwa mikono kutokana na mfumo wa IT kusumbua kwa takribani saa 1 uwanjani hapo.

Usumbufu uliojitokeza umepelekea pia tatizo la ratiba za ndege mtandaoni kuvurugika, japo mamlaka za uwanja huo ziliarifu kulimaliza tatizo hilo na kila kitu kuendelea kama ilivyo kawaida.

Heathrow

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

 

Tupia Comments