Mtandao wa Spotify wametangaza kuwa Taylor Swift ndiye msanii wa kwanza wa kike kupata streams zaidi ya milioni 100 ndani ya mwezi mmoja pekee.
Habari hizi zinakuja baada ya Taylor kutoa albamu yake ya tatu iliyorekodiwa upya mwezi Julai – Speak Now (Taylor’s Version) – ambayo ilishika nafasi ya kwanza katika chati za Marekani na Uingereza.
Pia ilimfanya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa na albamu nne katika chati ya albamu 10 bora kwa wakati mmoja – msanii wa tatu pekee EVER kufanya hivyo.
Ingawa anaweka rekodi za kwanza kwa wanawake, inamweka Taylor nafasi ya pili kwa jumla.
Rekodi ya wasikilizaji wengi zaidi wa kila mwezi kwenye programu inashikiliwa na The Weeknd yenye zaidi ya milioni 110 – rekodi ambayo aliweka mnamo Februari 2023.
Na nyota wa pop wa Uingereza Ed Sheeran ameshuka katika nafasi ya nne akiwa na rekodi ya milioni 77.