Habari za Mastaa

Taylor Swift kafikishwa Mahakamani kwa kuhusishwa na wizi… kinachofuatia?

on

Msanii wa muziki wa Pop kutoka Marekani, Taylor Swift anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za burudani baada ya msanii wa muziki wa R&B mwenye jina Jesse Braham kudai kuwa msanii huyo alimwibia mashairi ya wimbo alioutoa mwaka 2014 ‘Shake It Off’.

Jesse Braham amepeleka kesi yake Mahakamani na kwa mujibu wa mtandao wa Billboard wa Marekani, msanii huyo anadai fidia ya dola milion 42 ambayo kwa pesa ya Tanzania tunazungumzia kiasi cha kama Bilion 84 !… Jesse anadai kuwa aliuandika wimbo huo mwaka 2013 na kuupa jina la ‘Haters Gone Hate’ lakini Taylor aliuiba na kubadilisha baadhi ya mashairi.

SWIFT1

Taylor Swift.

Kingine anachodai Jesse Braham ni fidia ya gharama za uandishi ambapo anadai kuwa Taylor Swift hakubadilisha baadhi ya mashairi kwenye wimbo huo ikiwemo na jina la wimbo.

Nimekusogezea nyimbo zote mbili hapa chini, karibu uzicheki kuona kama kweli zinafanana mashairi.

Taylor Swift – Shake Off.

Jesse Braham – Haters Gone Hate.

https://youtu.be/808MLaHcBs4

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments